Mimi na wewe na vitu vyote ulimwenguni ni wazito kwa sababu ya 'Higgs Boson', inayojulikana pia kama 'The God’s Particle'. Wanasayansi wa CERN wamekuwa wakiitafuta 'higgs' (iliyojificha ndani ya 'higgs field') kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, kwa bajeti ya pauni za Uingereza bilioni sita. Chembe ya 'higgs' ikipatikana itawajulisha wanasayansi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa, na jibu la kitendawili cha 'Standard Model' litapatikana.