Usiwe na wasiwasi, Peter. Hizo ni hisia zangu tu. Huwezi kuwa mpelelezi. Lakini, kusema ule ukweli, ningependa sana kuonana na John Murphy. Kuna kazi binafsi ningependa kumpa. Wewe unatoka Afrika, hujawahi kumwona?” Debbie alizidi kumshtua Murphy. ...
Mlinzi mmoja wa ndani alishtuka aliposikia kishindo cha kitu kudondoka. Aligeuka upesiupesi lakini akaridhika alipokuta ni mwenzake ila akashindwa kuelewa kwa nini mwenzake huyo aanguke. Hata hivyo aliachana na Murphy na kuendelea na lindo lake huku ...
Watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi. Wanaheshimu nguvu ya matendo yako.
Radia Hosni alikuwa na bahati kuliko watu wote duniani. Frederik Mogens alipofika katika helikopta na kukuta Murphy na Yehuda wakihangaika kuutafuta mwili wa Radia, hakushangazwa na walichomwambia. Kwa sababu alijua nini kilitokea. Radia alikutwa aki...
Debbie alikuwa akimwangalia Murphy kama paka anavyoangalia maziwa.
Kolonia Santita imesambaa dunia nzima. Hapa Meksiko wana magenge rafiki zaidi ya mia moja yakiwemo makubwa kabisa katika Latino ya Matamolos na Baja California. Nikitekwa nyara na memba yoyote wa magenge hayo, kuna uwezekano mkubwa wasinifanye chocho...
Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” Debbie alisema akitabasamu. “Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais w...
Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila...
Lakini, akiendelea kuwaza na kuangaza, ghafla Murphy aliona kitu kama gari likiwa limesimama kwa mbali. Alisimama na kupata hamu ya kujua. Murphy alianza tena kutembea, lakini sasa akiifuata ile gari, halafu akaongeza mwendo na kukimbia; macho yote y...
Murphy alichanganyikiwa. Hakujua nini kilitokea na kwa nini. Ila, ghafla, alipotupa macho kushoto aliona kitu. Joka kubwa lilitambaa, ingawa kwa shida, kwa sababu ya sakafu, na kumfuata kummaliza. Murphy alijua joka hata angefanya vipi, hakuwa na uwe...
Majambazi huwapenda wanaowapenda. Chukulia mfano huu: Mimi na Wanda ni marafiki, OK? Baba yake, au genge la baba yake, hataweza kunidhuru au kuwadhuru watu ninaowapenda kwa sababu tu ya urafiki na mtoto wake. Na yeye anaweza kufumbiwa macho akifanya ...
Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hal...
Saa nane za usiku timu nzima ya Vijana wa Tume ilirudi San Ángel katika helikopta ya DEA, tayari kwa safari ya Salina Cruz katika jimbo la Oaxaca. Kukamatwa kwa Gortari, Eduardo na Dongyang ulikuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa Tume ya Dunia. Ushindi ...
Mapema, kabla ndege haijaondoka na baada ya kuagana na maafisa waliomsindikiza, Nanda aliingia katika ndege na kutafuta namba ya kiti chake. Alivyoiona, alishtuka. Msichana mrembo alikaa kando ya kiti (cha Nanda) akiongea na simu, mara ya mwisho kabl...
Nusu dakika baada ya kuondoa gari, Murphy aliona kiwiliwili cha mtu kikimwendea mbio kutokea katika nyumba ya magaidi! Hapohapo alisimamisha gari na kuacha taa zikiwaka, halafu akashika bunduki na kushuka – akiwa ameangalia mbele kwa tahadhari kubw...
Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu. “Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa. “Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi. “60111...
Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre ya kubadil...
Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya ...
Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (‘Ghillie Suits’) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migong...
Sigara zilizidi kuvutwa, ndani ya nyumba, na magaidi wale wawili, wakati Murphy akisinzia kudanganyia kama kweli nguvu zilishamwisha. Alimfikiria tena mpenzi wake Sophia, safari hii sana. Alimkumbuka Debbie; hakujua alikuwa wapi na hakujua mama yake ...