Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa. Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.