Quote by: Enock Maregesi

Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.


Share this: