Quote by: Enock Maregesi

John Murphy amefariki dunia. Ndege aliyotoka nayo hapa, Dar es Salaam, ndiyo aliyotoka nayo Paris na ndiyo hiyo iliyoanguka katika mazingira ya kutatanisha. Watu waliobahatika kuing’amua fununu hii ni wachache na ambao hivi sasa hawajiwezi kabisa, akiwemo kamishna wetu wa kanda Profesa Mafuru. Profesa yuko mahututi. Ameshtuka baada ya kusikia taarifa hizo katika redio ya hapa. Yuko chini ya uangalizi mkali wa madaktari. Mungu aiweke roho ya John Murphy, shujaa wa karne, mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.


Share this: