Quote by: Enock Maregesi

Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu. “Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa. “Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi. “60111906,” Mogens alisema, baada ya sekunde kumi. “57121906,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi. “Jumapili,” Mogens aliendelea, baada ya sekunde kumi. “Ijumaa,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi. John Murphy wa Kolonia Santita aliposema ‘Ijumaa’, Mogens aliunda kicheko na kurusha mkono katika matundu ya kuongelea ya simu ...


Share this: