Quote by: Enock Maregesi

Mlinzi mmoja wa ndani alishtuka aliposikia kishindo cha kitu kudondoka. Aligeuka upesiupesi lakini akaridhika alipokuta ni mwenzake ila akashindwa kuelewa kwa nini mwenzake huyo aanguke. Hata hivyo aliachana na Murphy na kuendelea na lindo lake huku akivuta msokoto mfupi wa bangi. Lakini, yule mlinzi hakutembea hatua nyingi kabla ya kusimama na kujiuliza maswali kichwani. Kwa nini mwenzake huyo atoke nje ambako ndiko alikuwa amepangiwa na ambako ndiko waliambiwa kuwe na ulinzi imara na ndiyo maana wakawekwa saba? Kwa nini aanguke ndani ya ua bila hata ya kumsemesha chochote? Kwa nini hakumpigia redio kwamba alikuwa akiingia ndani ili asiwe na wasiwasi? Alipowaza sana aliamua asiwe na pupa. Aliamua kumfuata mwenzake, aliyekuwa mbele yake, ili amwambie kitu na washirikiane.


Share this: