Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.
Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD – Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia – ili iendelee kuimarisha hudu...
Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya...
WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa y...
Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Isra...
Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita...
Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauli...
Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.
Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashari...
Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu. “Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa. “Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi. “60111...
Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya ...
Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre ya kubadil...
Kuna vita za aina mbili zinazopiganwa hapa duniani: vita ya maisha na vita ya dhambi. Unaweza kushinda vita ya maisha (maisha ya raha) lakini ukashindwa vita ya dhambi (maisha ya laana). Kushinda vita ya dhambi ni lazima umkaribishe Mwana wa Mungu Mf...
Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsaf...
Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwis...
Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) n...
Kujua ukweli juu ya uraibu wa madawa ya kulevya kunaweza kumsaidia mtu kujua madhara ya madawa ya kulevya.
Wakiwa na suti nzito za kijani na madoa meusi (‘Ghillie Suits’) kwa ajili ya kupigania porini; Vijana wa Tume walikuwa na kofia za chuma, miwani ya kuonea usiku (iliyokuwa na uwezo wa kubinuka chini na juu), redio na mitambo ya mawasiliano migong...
Ukitaka kuwa mfanyabiashara mzuri wa madawa ya kulevya usitumie madawa ya kulevya. Siri ya mafanikio ya Kolonia Santita ni nidhamu na kitalifa.
Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utat...
Usiifundishe familia yako anasa. Ifundishe upendo, unyenyekevu na hofu ya Mungu. Ukiifundisha anasa utahatarisha maisha ya mbinguni ya familia yako, na ya kwako pia.