Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu.
Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwe...
Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.
Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.
Ramachandra maana yake ni mwezi. Mwezi ni setilaiti na mwezi unamulika. Ramachandra anaitwa setilaiti kwa sababu ya umuhimu wake katika bara la Asia. Anamulika India na bara zima la Asia, na Australia, kwa niaba ya Kolonia Santita. Ana miaka 44. Ana ...
Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita...
Kama mwanadamu una haki ya msingi kuwa na amani katika maisha.
Watu wanapokuwa katika migogoro maisha yao hutakiwa kurahisishwa. Kuna ukingo mwembamba kati ya uzima na wazimu.
Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani!
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, masaa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safiri salama.
Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC.
Nje ya uwezo wa kisheria ni shetani.
Wasifu wa viongozi wa Kolonia Santita ni siri kwa sababu siri ni siri ya mafanikio.
Wanaume hujiua kwa sababu ya fedha. Wanawake hujiua kwa sababu ya mapenzi.
Usuluhishi ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu.
Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake.
Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD – Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia – ili iendelee kuimarisha hudu...
The best prize life has to offer is not a chance to work hard and be something in the community. It is the perfume of God that resides within you.
Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo.
Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio.