Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.